Sunday, October 23, 2016

FAIDA YA MBOGA SPINACHI NA VIAZI

Faida ya Kula spinachi na viazi

Imebainika kuwa ulaji wa matunda na mbogamboga zenye kimeng’enyo cha carotenoid kwa wingi kama vile karoti, spinachi, tikitiki maji na hata viazi vitamu, unaweza kuondoa katika
hatari ya kupata magonjwa kupitia viondoa sumu vinavyopatikana ndani yake.

Watafiti kadhaa wameitaja carotenoid kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin A. miongoni mwa sifa kuu ya kimeng’enyo hicho ni kuukinga mwili dhidi ya maradhi makubwa yakiwemo shinikizo la damu pamoja na saratani ya matiti.

Mtafiti kiongozi wa chuo kikuu cha afya za jamii Harvard, caroline Boeke amelianmbia jarida la HealthyDaily kwa tafiti nyingune zimeonyesha athari za matunda na mbogamboga pamoja na carotenoid iliyomo ndani yake kwa afya ya matiti.

Nyingi kati ya tafiti hizo zilionyesha matokeo mchanganyiko, lakini kwa ujumla wale zilishauri kuwa kimeng’enyo cha carotenoid inayopatikana kwenye mbogamboga na matunda yenye chembechembe za rangi ya njao, machungwa au nyekundu ina matokeo chanya kwa afya ya matiti.

Katika utafiti huo uliokuwa ukifanywa tamgu mwaka 1996, kwa kupitia ripoti ya vyakula waliyokuwa wakitumia hadi mwaka 1998 na kasha kufanya tathimini mwaka 2005, 2007 na mwaka 201o ilibainika kuwa wasichana wengi waliotumia mboga hizo hawakuwa nadalili zozote za kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wale ambao walikuwa hawatumii.
mgblog

No comments:

Post a Comment