Wednesday, October 26, 2016

MTU MTI KIVUTIO MITAA YA MAREKANI

Mtu aliyevalia kama mti akamatwa Marekani

rMatawi
Mwanamume aliyefunikwa kwa matawiMtu mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama "binadamu mti", alikamatwa baada yake kuvuka barabara akiwa amevalia kama mti.
Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi
Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa "yananukia".
Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?
"Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini.
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.

No comments:

Post a Comment