Friday, October 21, 2016

CHOMBO KILICHOENDA MARS CHATOWEKA

Sababu ya chombo cha Ulaya kutoweka Mars

Sehemu ya ndani
Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) ambalo lilituma chombo cha anga za juu kwa jina Schiaparelli limeeleza sababu ambazo huenda zilichangia chombo hicho kutoweka Jumatano.
Chombo hicho kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo lakini mawasiliano yakakatika ghafla na kuzua wasiwasi.
Maafisa sasa wanasema parachuti (mwavuli) ambayo ilifaa kutumiwa na chombo hicho kutua salama ilitengana na chombo hicho mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Aidha, roketi ambazo zilifaa kusaidia chombo hicho kusimama angani muda mfupi kabla ya kufika kwenye 'ardhi' ya Mars pia ziliwaka kwa muda mfupi sana kuliko ilivyofa
Uamuzi huo umetokana na data ambayo roboti iliyo kwenye chombo hicho cha Schiaparelli iliweza kutuma kwa chombo mama kwa jina Trace Gas Orbiter (TGO) ambacho kilibaki kikiizunguka sayari hiyo.
Maafisa wa ESA wanasema kufikia sasa bado hawajakata tamaa kabisa kuhusu hatima ya chombo hicho, ingawa hawana matumaini sana.
Kuna uwezekano kwamba chombo hicho kilifikia sayari hiyo kikienda kwa kasi isiyofaa na hivyo kikaharibika.

No comments:

Post a Comment