Sunday, October 16, 2016

WATOTO WALIOSHIKANA VICHWA , WATENGANISHWA

Pacha walioshikana kichwani watenganishwa New YorkWavulana pacha

Wavulana wawili pacha ambao walikuwa wameshikana vichwani wametenganishwa na madaktari mjini New York, Marekani.
Jadon na Anias McDonald wa umri wa miezi 13 walifanyiwa upasuaji uliochukua saa 16 katika hospitali ya Montefiore.
Kwa sasa wanafanyiwa matibabu ya kuwezesha mafuvu ya vichwa vyao kukua na kujaza pengo lililoachwa.
Mama yao Nicole McDonald aliandika kwenye Facebook Ijumaa asubuhi jinsi alivyokuwa na furaha lakini pia na "uchungu kuhusu mustakabali wa watoto hao.
Alipakia picha ya Jadon akiwa peke yake kitandani.
"Hata niliwauliza mbona walipanga upya chumba cha kulala kwa sababu haikuwa imeniingia akilini kwamba ningehitaji kitanda cha ziada," McDonald aliandika.
Alisema wasichana hao ni kama wamezaliwa upya.
BBC

No comments:

Post a Comment