Thursday, October 20, 2016

MATAIFA YENYE WEREVU ZAIDI DUNIANI

Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani

University of Sydney
Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?
Jambo la kushangaza ni kwamba orodha hii inaonyesha taswira tofauti sana na ile inayotolewa na utathmini wa vyuo vikuu.
Shirika la Kimataifa la Uchumi na Maendeleo (OECD) limefanya wazi matokeo ya mtihani wa kupima uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kutoka nchi mbalimbali.
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uingereza kama vile Harvard, MIT, Stanford, Oxford, Cambridge na UCL.
Lakini baada ya OECD kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu, wanafunzi walio bora zaidi ilibainika wanatoka Japan na Finland na wala si Marekani na Uingereza..
Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanaohitimu kwa mujibu wa OECD
  1. Japan
  2. Finland
  3. Uholanzi
  4. Australia
  5. Norway
  6. Ubelgiji
  7. New Zealand
  8. England
  9. Marekani
  10. Jamhuri ya Czech
Nchi hizi zote huwa mara nyingi hazina chuo haka kimoja kinachokuwa kwenye orodha ya vyuo vikuu 10 bora duniani.
Badala ya vyuo vikuu vya Marekani kufana, yamkini vyuo vikuu vya Norway na Australia vina wanafunzi bora wanaohitimu.
Kwa mujibu wa orodha ya ubora wa vyuo ya QS World University Rankings, kulikuwa na vyuo 32 vya Marekani katika 100 bora, na chuo kikuu kimoja pekee kutoka New Zealand.
Lakini ripoti ya OECD inaonesha wanafunzi wa New Zealand wanafanya vyema kushinda wenzao Marekani.
Image copyright iStock
Image caption Oxford kilirodheshwa kuwa chuo kikuu bora duniani kwenye orodha ya gazeti la Times
Image copyright iStock
Image caption Wanafunzi waliohitimu kutoka Japan walifanya vyema zaidi tathmini ya OECD
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu ya QS 2016-17
  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford University
  3. Harvard University
  4. University of Cambridge
  5. California Institute of Technology (Caltech)
  6. University of Oxford
  7. University College London
  8. ETH Zurich
  9. Imperial College London
  10. University of Chicago

No comments:

Post a Comment