Monday, October 17, 2016

KINDA WA NIGERIA ALIEKUWA AKIWANIWA ULAYA AUWAWA

Mchezaji wa Nigeria apigwa risasi na kufariki

Mchezaji wa shooting Stars nchini Nigeria Izu Joseph kushoto
Mwanasoka  anayesakata dimba katika michuano ya ligi ya Nigeria, amepigwa risasi na kufariki nyumbani kwake katika jimbo la Bayelsa kusini mwa nchi hiyo.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa Izu Joseph, beki wa timu ya Shooting Stars, aliuawa na askari waliokuwa wakikabiliana na wanamgambo katika eneo lenye utajiri wa mafuta.
Miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano mapya katika eneo la Delta, huku wapiganaji wakitaka kupewa sehemu ya utajiri wa mafuta.
Mwanasoka huyo ambaye likuwa akiwaniwa na klabu nyingi za Ulaya ndoto zake zimezima baada ya kupigwa riasi na kufariki papo hapo leo.
IZU kushoto wakati wa uhai wake akiwa uwanjani kama anavyoonekana .

No comments:

Post a Comment