Thursday, October 27, 2016

FA YAMSHITAKI MOURINHO KWA KAULI CHOCHEZI

Mourinho ashtakiwa na FA kwa kumuingilia refa

Jose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudai kwamba itakuwa vigumu kwa refa Anthony Taylor kusimamia mechi yao dhidi ya Liverpool.
Mourinho aliongeze kwamba kumteua Taylor kusimamia mechi hiyo ya tarehe 16 Oktoba ilimpatia shinikizo refa huyo mwenye makao yake Manchester.
Mameneja hawaruhusiwa kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi.
Mourinho ana hadi Oktoba 31 kujibu shtaka la ukosefu wa nidhamu na kusababisha mechi hiyo kuwa na jina baya.
Taylor alito kadi 4 za njano zote kwa timu ya Manchester United katika sare hiyo ya 0-0

No comments:

Post a Comment