Saturday, October 29, 2016

MWANAMKE ALIE NA MACHO YA AJABU AKAMATWA

Mwanamke mwenye 'macho ya kushangaza' akamatwa.Steve McCurry na picha za Sharbat Gula Hamburg, Ujerumani Juni 27, 2013.

Mhamiaji kutoka Afghanistan, ambaye alipata umaarufu picha yake ilipochapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa jarida la National Geographic miaka thelathini iliyopita, amekamatwa.
Maafisa wanasema amekamatwa kwa kuwa na nyaraka bandia za utambulisho.
Sharbat Gula alipata umaarufu mwaka 1985 kutokana na picha hiy aliyopigwa akiwa na umri wa miaka 12.
Macho yake yalikuwa na rangi ya kijani, jambo lililomfanya kufahamika kwa jina 'Green-eyed Girl'.
Maafisa wanasema alikamatwa na Idara ya Uchunguzi ya Pakistan (FIA) baada ya uchunguzi wa miaka miwili Peshawar, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
Pakistan ilianza kuwasaka watu wenye vitambulisho bandia majuzi.
 Gula aliwasilisha ombi la kutaka kitambulisho Aprili 2014 akitumia jina Sharbat Bibi.
Iwapo madai hayo yatathibitishwa, basi atakuwa mmoja wa maelfu ya wakimbizi kutoka Afghanistan ambao wamejaribu kukwepa mfumo wa usajili wa watu unaotumia kompyuta nchini Pakistan.
Afisa wa Mamlaka ya Taifa ya Usajili wa Watu (Nadra) amesema maafisa wa FIA pia wanawatafuta wafanyakazi watatu ambao wanadaiwa kumpa kitambulisho Bi Gula.
Gazeti la Dawn la Pakistan limesema  Gula alipewa vitambulisho pamoja na wanaume wengine wawili waliodai kuwa wanawe wa kime

No comments:

Post a Comment