Wednesday, October 19, 2016

ARSEANAL YAFANYA KWELI UEFA

Uefa: Barcelona yaiua Manchester City ya kocha wake wa zamani

Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya
Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnonoMichuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.
Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu
Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.

Matokeo ya michezo mingine

Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven
Paris Saint-Germain 3-0 Basel
Dynamo Kiev 0-2 Benfica
Napoli 2-3 Besiktas
FC Rostov 0-1 Atlético Madrid

No comments:

Post a Comment