Monday, October 17, 2016

CHINA YATUMA WATAALAMU ANGA ZA JUU

China yatuma wana anga kwenye mzingo wa dunia

Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 kilibebwa na roketi kwa jina Long March-2F ambayo ilirushwa kutoka mkoa wa Gansu kaskazini mwa China JumatatuChina imerusha roketi ambayo inawabeba wana anga wawili ambao wataenda kwenye kituo chake cha anga za juu kinachozunguka kwenye mzingo wa dunia.
Wana anga hao waliondoka kutoka chumba cha kurushia roketi na satelaiti cha Jiuquan kaskazini mwa Uchina.
Watatua katika kituo cha anga za juu cha Tiangong 2 ambapo watakaa siku 30, hicho kikiwa kipindi kirefu zaidi ambacho wana anga wa China wamekaa katika anga za juu
Uzinduzi huo na miradi mingine iliyozinduliwa awali ni ishara za kujiandaa kwao kutuma watu Mwezini au katika sayari ya Mars.
Kituo cha awali cha anga za juu kilichoitwa Tiangong, Kasri la Mbinguni, kilifungwa mapema mwaka huu baada ya kupokea roketi tatu.
Wana anga walio kwenye roketi iliyorushwa sasa ni Jing Haipeng, 49, ambaye amewahi kwenda anga za juu awali mara mbili, na Chen Dong, 37.

No comments:

Post a Comment