Thursday, October 20, 2016

HADITHI, YAMENIKUTA SALMA MIE SEHEMU 22

HADITHI
 
YAMENIKUTA SALMA MIE  22
 
ILIPOISHIA
 
“Kwani ana tatizo gani?” akaniuliza.
 
“Ni uzee tu. Kila mahali panamuuma. Na presha yake pia iko juu” nikadanganya. Kwa kuwa sikutaka tuendelee na mazungumzo yale nikamuuliza. 
 
“Kaka yako ameshalala?” nikamuuliza Zacharia.
 
“Ameingia chumbani muda mrefu”
 
“Mmekula nini?”
 
“Tumekunywa chai. Nilikwenda kununua mkate”
 
Nikajidai kumuuliza  “Mmenibakishia na mimi?”
 
“Tumekuachia silesi zako”
 
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
 
Baada ya hapo tukabaki kimywa tukiangalia ile kanda. Kukaa kwangu pale na kuangalia ile kanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua nilikuwa nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda dhambi.
 
Ghafla Ibrahim akatoka mle chumbani na kumuuliza mdogo wake.
 
“Shemeji yako hajarudi hadi muda huu?”
 
SASA ENDELEA
 
Bila kupenda niliangalia ile kanda, hadi ilipokuwa inakaribia kwisha Ibrahim akatoka na kumuuliza zacharia..
 
“Shemeji yako hajarudi bado?”
 
Chinga akapiga funda jingine la bia. Alipoirudisha bilauli aliniambia.  “Hatutakosa njia nyingine. Nakupa muda uendelee kufikiri lakini jaribu kumshinikiza akupe talaka”
 
“Wewe utakuwa hapa Tanga mpaka lini?”
 
“Sina muda mrefu. Naweza kuondoka siku yoyote nitakayoamua”
 
“Basi tuendelee kufikilia njia nyingine. Kwa vile sina nia ya kuendelea kuishi naye kama hata niacha yeye nitamuacha mimi!”
 
“Lakini umenipenda?” Chinga akaniuliza ghafra. Macho yake yalionesha kuwa ulevi ulikuwa umeanza kumchukua.Iliwezekana alianza kunywa muda mrefu.
 
“ Kama nisingekupenda nisingekuja huku” nikamjibu
 
“ Kama ni kweli kunywa bia kidogo”
 
“Nimekuambia situmii”
 
“Onja kidogo”
 
“Nitaonya siku nyingine”
 
“Basi njoo uketi hapa”
 
Alimaanisha nikaketi naye kitandani.
 
“Hapa nilipokaa panatosha”
 
Chinga akainuka na kunifuata akanishika mkono na kuniinua. 
 
‘Mbona uko hivyo Salma? Hebu twende tukakae pale”
 
“Chinga utasababisha nichelewe nyumbani” nikajidai kulalamika huku nikimfuata kwenye kitanda. Nikaketi na yeye akaketi”
 
“Wewe umeshaamua kuwa na mimi unajali nini kuchelewa. Wewe ni wangu tu au si kweli?”
 
Nikanyamaza kimya na kubaki kumtazama machoni.
Akatabasamu na kunipitishia mkono kiunoni  “Una macho ya kimahaba kweli!” akaniambia kisha akanibusu midomoni.
 
Kilichofuatia baada ya hapo sitakisema. Ni aibu
 
Ilikuwa saa nne ikikaribia kuwa na nusu Chinga aliponirudisha nyumbani. Nilimwaambia asimamishe gari nyumbni kwa Mwanaisha ili Ibrahim na mdogo wake wasijue kuwa nimeletwa na gari
 
Chinga akanipa shilingi laki moja kabla sijashuka kwenye gari
 
“Ahsante” nikamwaambia kabla ya kuagana naye. Nikashuka na kutembea kuelekea nyumbani. Niliposhuka tu Chinga akaondoka na gari
 
Nilipofika nyumbani mlango wa mbele ulikuwa umefungwa.Nikabisha.Abdul akaja kunifungulia, nikaingia
 
“Habari ya saa hizi?” akanisalimia
 
“Nzuri” nikamjibu huku nikizuga kwa kuangalia kwenye luninga
 
“Unatazama kanda?” nikamuuliza
 
Niliona deki imewashwa na kuonyesha filamu za akina Kanumba.
 
“Ndiyo shemeji” Abdul akanijibu huku akifunga mlango.
 
“Unamuonaje shangazi?’
 
“Bado anaumwa” nilimjibu huku nikiketi kwenye sofa.
 
Nikajifanya nataka kuangalia ule mkanda
 
Abdul aliondoka kwenye mlango naye akaja kuketi
 
“Tatizo la shangazi ni nini?” akaniuliza
 
“Ni uzee tu. Kila mahali panamuuma.Na presha yake pia iko juu” nikadanganya.Kwakuwa sikutaka tuendelee na mazungumzo yale nikamuuliza  “Kaka yako ameshalala?”
 
“Ameingia chumbani muda mrefu”
 
“Mmekula nini?”
 
“Tumekunywa chai.Nilikwenda kununua mkate”
 
Nikajidai kumuuliza  “Mmenibakishia na mimi?”
 
“Tumekuachia silesi zako”
 
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
 
Baada ya hapo tukabaki kinywa  tukiangalia ule mkanda.Kukaa kwangu pale na kuangalia huo mkanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua nilikuwa nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda hatia.
 
Bila kupenda niliuangalia ule mkanda hadi ulipokuwa unakaribia kwisha Ibrahim akatoka na kumuuliza Abdul. “Shemeji yako hajarudi bado?”
 
ITAENDELEA kesho hapahapa usikose uhondo huu

No comments:

Post a Comment