Thursday, October 20, 2016

MGAMBO JKT JINO KWA JINO NA MVUVUMA FC YA KIGOMA



Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA Mkuu wa Mgambo JKT, Athuman Cairo , amewataka wachezaji wake kufanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni ili kujiweka sawa kuweza kukabilia na mchezo wao na Mvuvuma FC ya Kigoma   kesho  uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi uwanja wa Mkwakwani jana, Kaira alisema hataki kurejea makosa yaliyoilazimisha timu yake kutoka kutoka suluhu ya kufungana bao moja moja.
Alisema yuko makini kuwaangalia wachezaji wake katika kila aina ya mazoezi yakiwemo ya viungo na kasi ya uwanjani pamoja na kuwahi mazoezi kwa wakati hivyo kuahidi kupata ushindi mnono.
“Kwa sasa nimefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza wakati wa mechi yetu iliyopita na kulazimishwa kutoka sare, nimewaeleza kuwa nitakuwa mkali kuona mchezaji hafuati maelekezo ninayotoa” alisema Caoro na kuongeza
“Natambua ligi hii ni ngumu na kila timu imesajili wachezaji wazuri na kujipanga, niko na imani na kikosi change lakini sitobweteka nataka kila mmoja kujua wajibu wake uwanjani” alisema
Aliwataka washabiki wa mpira Tanga kuishangilia timu yake uwanjani kwa wingi ili kuipa na kuzipa hamasa timu za Tanga ili kurejesha makali yake kama ilivyokuwa msimu wa ligi uliopita.
Aliwataka kusahau machungu ya timu za Tanga kushuka daraja na badala yake kuzipa moyo na hamasa kwa kujitokeza kw awingi uwanjani kwa kuzishangiliwa kwa kutambua kuwa timu za Tanga ni za wana Tanga na zitaendelea kuwa za wana Tanga.
Kwa upande wake, Kaptaini wa timu hiyo, Shai Mpala, alisema wamejipanga vyema kuikabili Mvuvuma na kusema kuwa pointi tatu zitabaki Mkwakwani ambapo hakuna majeruhi hadi muda huo.
Alisema mazoezi na maelekezo ambayo wamekuwa wakipatiwa na makocha wao wamekuwa wakiyazingatia hivyo kuomba uzima hadi siku hiyo kwa madai kuwa wako na hamasa.
“Tuko na hamasa na shauku ya mchezo ulioko mbele yetu na nina imani kuwa kwa tulivyoiva ushindi utabaki hapahapa uwanjani, washabikiw awasiwe na hofu ninachowataka wajitokeze kwa wingi.
Alisema ili kuweza kuibuka na ushindi amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi siku ya mechi ili kuwapa mori wachezaji uwanjani na kuwashangilia kwa nguvu.
                                                   Mwisho

No comments:

Post a Comment