Mwanamuziki raia wa Rwanda aliye na hofu ya kurudi nyumbani
Mwaka 1994 alikuwa na umri wa miaka 17 akiishi
nchini Rwanda kwenye familia moja tajiri na ndoto yake ilikuwa ni ya
kuwa muimbaji maarufu.Lakini maisha ya Corneille Nyungura yalichukua mkondo mwingine kwa ghafla wakati yalitokea mauaji ya kimbari ya mwaka mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000 wa kabila la watusi na wahutu wachache wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Wakati kundi la wauaji lilipowasili nyumbani kwao, Corneille alijificha nyuma ya sofa wakati familia yake yote ilichinjwa.
Akijaribu kukubaliana kile kilichotokea nchini mwake mwaka 1994, Corneille anasema kuwa na uoga wa kurudi nyumbani kwao.
No comments:
Post a Comment