Saturday, October 8, 2016

WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA PSPF KWA WALIMU WASTAAFU TANGA YAFANA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akizungumza na wanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja jana. kulia anaemwangalia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akipokea Hati na Katiba ya Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) kutoka kwa aliekuwa Afisa Elimu shule ya Msingi jiji la Tanga, Damass Kifanga.


Wanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu  jiji la Tanga (Chawajita) , wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF), Adam Mainga, wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja kwa walimu wastaafu uliofanyika Tanga jana.



  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, akifungua mkutano wa wanachama wa Chama Cha  Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chawajita) wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) uliofanyika Tanga
  Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chajiwata)  Debora Daffa, akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika Tanga jana.
  Mwanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) Roda Matoi, akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) na walimu wastaafu wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja na kufanyika ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga jana




Viongozi wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) pamoja na STAFF ya Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella mara baada ya mkutano na walimu wastaafu wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika jana ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.

No comments:

Post a Comment