Tuesday, July 21, 2015

MWENGINE AJITOKEZA KUMPOSA MALIA OBAMA

Mwingine kajipanga na posa ya ng’ombe kumpata Malia Obama, ataweza?

DSCI0095
Hivi kweli Malia Obama atakubali kupata mpenzi toka Kenya kisa baba yake ana asili ya huko?
Iliwahi kuchukua headlines stori ya jamaa ambaye kazi yake ni Wakili, alitangaza kabisa mpaka posa ya ng’ombe na mbuzi ambao amejipanga nao kutoa posa ili ampate Malia.. leo ni mwingine, kazi yake ni mfugaji na yeye kajiandaa kabisa na ng’ombe kama 500 hivi alafu anasema hata zikitakiwa zaidi wako tayari kuongeza.
DSC III
>>>> ‘Tumekusanya ng’ombe 500 wakitaka zaidi tuko tayari kutoa… sina mchezo kabisa niko serious, hizi ng’ombe naweza kuzipakia kwenye meli na ziende‘>>>> Jeff Ole Kishau.
Basi akaulizwa kama ataweza kuongeana Malia kwa kiingereza, jibu lake hili hapa >>> ‘Najua kiingereza kidogo siwezi kushindwa.. naweza kuongea ‘YES how are you Malia’… ataelewa kabisa’ >>> Jeff Ole Kishau.
DSC II
Unaambiwa hata ndugu na jamaa zake wanaamini jamaa atampata Malia Obama >>>> ‘Hata yeye mwenyewe (Obama) ni damu ya Kenya, alienda Marekani akajenga akapata familia mbegu ikaenea huko, tunaomba atupe huyo msichana ili arudishe mbegu Kenya‘ >>>> Mmoja wa wazee ambao wanatoka Kijiji ambacho anatoka Jeff Ole Kishau.
Zimebaki siku chache Rais Obama atue Kenya, najua zitakuwepo stori nyingi kila wakati kwa sababu ya ugeni huo… nitahakikisha zote zinakufikia pia hapahapa on Tangakumekuchablog mtu wangu.

No comments:

Post a Comment