Utaratibu mpya Korea ikifika saa 11 Alfajiri kila mtu anatakiwa kuwa Ofisini… Wataiweza kweli?
Headlines toka Korea Kaskazini sasa hivi
ni kwamba hali ya hewa ni joto sana, lakini yapo mengine toka huko
ambapo msimu huu wa joto kali umepewa jina la Sambok.
“Ofisi
zote, shule, na kila taasisi nchi nzima zinatakiwa kufuata ratiba mpya
ambayo Serikali imeweka… Ratiba kwa sasa ni kwamba kila kitu kitaanza
kufanya kazi saa 11 asubuhi badala ya saa mbili asubuhi, na mwisho wa
shughuli zote ni saa saba mchana” >>>> Hii ni sehemu ya agizo hilo jipya la Serikali ya Korea Kaskazini.
Wastani wa joto la Korea ni kama 29˚
Centrigrade, lakini kwa sasa imefikia mpaka 40˚ Centigrade… Hii sio mara
ya kwanza kutangazwa utaratibu huo, wakati Rais Kim Jong-il akiwa madarakani iliwahi kutangazwa utaratibu wa aina hii pia.
Noma nyingine ni kwamba Maofisini kwenye
AC na feni huenda hii isiwe taarifa nzuri kwao, joto limekuwa kali na
hakuna maji ya kutosha kwenye vyanzo vya umeme sasahivi, kwa hiyo ishu
ya feni na AC kufanya kazi ofisini huenda ikawa kitendawili kigumu
kuteguka.
“Kwa maana
hiyo wanafunzi watatakiwa kuamka na kuanza kujiandaa saa kumi usiku,
hiyo ni ngumu sana na wakati mwingine unakuta watoto wanakosa vipindi
viwili au vitatu kila siku” >>>> Huyu ni mmoja wa watu ambao hawajapenda kabisa huu utaratibu.
Watu wengi hawajapenda hiyo ratiba mpya,
unaambiwa mpaka Migahawa ya Serikali inatoa huduma mwisho mchana,
ukienda jioni au usiku hakuna huduma utakayopata !!
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment