Pilikapilika za Nairobi wanavyojiandaa kumpokea Obama… (Pichaz)
Rais Obama na Familia yake, hii ni kama TBT hivi… picha moja ya zamani zamani kabisa.
Kila ukiingia kwenye Mitandao ya Kijamii Kenya stori nyingi kubwakubwa na zenye headlines ni kuhusu ujio wa Rais Obama.. sio kitu kigeni kwa sababu hata alivyokaribia kuja TZ stori zilikuwa nyingi vilevile na zinazofanana na hizo.
Leo nimekutana na pichaz nyingine pamoja na stori nyinginyingi kuhusu Nairobi na ujio wa Obama.
Kogelo kuna hii Shule ambayo imepewa jina la ‘Senator Obama Primary School‘
Achana na jina la Shule mtu wangu, wako watoto ambao wamepewa jina la Barack Obama, hili ni daftari la mwanafunzi anaitwa ‘Barack Obama Okoth‘
Kama kawaida, mtaani wako jamaa ambao biashara yao ni kuuza hizi Bendera.
Hukohuko mtaani kuna kuta tayari watu wa graffiti wameshapita kupendezesha namna hii.
Wengine wamekamata fursa ya kutengeza tshirt na biashara inaendelea kona kona za Nairobi !!
Mgeni njoo…. haya, barabara zinaendelea kuwekwa sawa mambo yasiharibike mgeni akija.
Kuna barabara ziko free kabisa na nyingine ni foleni mpaka basi !! Kuna barabara ambazo zitafungwa ili kuacha msafara wa Rais Obama upite huko salama kabisa.
Watu na vipaji vyao, fursa nyingine ni hii aliyoikamata huyu jamaa, kachora picha kali sana ya Obama na Kenyatta wanakula ugali samaki !! Mpaka vibuyu viko mezani..
Usikae mbali nami nitakuhabarisha kila linalojiri Nairobi mwanzo mwisho ujio wa Rais wa Marekani Barak Obama
No comments:
Post a Comment