Tuesday, July 28, 2015

MTOTO WA RAIS WA ZAMANI WA LIBYA AHUKUMIWA KUNYONGWA

Hii ni hukumu iliyotolewa leo JULAI 28 na mahakama ya Libya kwa mtoto wa Gaddafi …

coti
Mahakama ya  Libya leo imetoa hukumu kwa mtoto wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Gaddafi, aitwaye Saif al Islam na wenzake nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011.
Wote walikuwa wameshtakiwa pamoja sasa wamehukumiwa kunyongwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kazima maandamano wakati wa mapinduzi hayo.
son
Mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi aliyehukumiwa kunyongwa
Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia kanda ya video.
Kwa sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan ambapo wamekataa kumuachilia huru.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment