Saturday, July 25, 2015

JE, UNAJUA ARSENAL ILIWAHI KUZAWADIWA KOMBE LA DHAHABU? KWA NINI, YOTE YAPO HAPA

Unaukumbuka Ushindi wa Arsenal wakapewa na Kombe la dhahabu? Cheki pichaz

Arsenal_logo-3 (1)
Nimeona nikusogezee moja kati ya rekodi ambazo klabu ya Arsenal iliwahi kuziweka mwaka 2004 chini ya kocha Arsene Wenger ambaye yupo hadi sasa akiifundisha klabu hiyohiyo… Wenger bado ana heshima ya kipekee Emirates licha ya kuwa kwa miaka ya hivi karibuni hajaleta mafanikio makubwa kwenye Klabu hiyo.
img_9064
May 2004 waratibu wa Ligi Kuu Uingereza walilazimika kutengeneza Kombe maalum la Ligi Kuu kwa ajili ya Klabu ya Arsenal, hiyo ilifanyika baada ya Arsenal kuandika rekodi ya kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja msimu wa 2003-04.
936061_w2
Upekee wa Kombe walilopewa Arsenal msimu huo ilitokana na Bodi ya Ligi Kuu kuandaa Kombe lenye material ya dhahabu, hii ilikuwa tofauti kabisa na haikuwahi kufanyika kitu cha aina hiyo siku za nyuma na halikuwahi kutolewa Kombe la aina hiyo tena mpaka sasahivi.
article-0-00D9F63A0000044C-316_468x462
Hata hivyo huo ulikuwa ni wakati ambao kikosi cha Arsenal kilikuwa kikibebwa na mastaa kama Thierry Henry, Patrick Vieira, Dennis Bergkamp, Nwankwo Kanu, Robert Pires, Ryan Smith, Sol Campbell na Reyes na wengine wengi huku makocha wakiwa Arsene Wenger na msaidizi wake Boro Primorac.
1413462733044_lc_galleryImage_Arsenal_soccer_fans_crowd
Arsenal_open_top_bus_parade_2004
Hii ndio Video inayoonesha jamaa walivyoupata huo ushindi wao 2004.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment