Tangakumekuchablog
Tanga, WAKAZI
wa kijiji cha Majimoto kata ya Mafuriko halmashauri ya jiji la Tanga,
wameshangazwa na Wizara ya Utalii na Maliasili kuacha kuifanya chemchem inayotoa maji moto iliyoko kijiji hapo kuwa ya kitalii hatua ambayo inaikosesha Serikali mapato.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
jana, wakazi hao walisema Chemchem hiyo imekuwa kivutio jambo ambalo wageni
kutoka mataifa ya nje hufika na kujionea maajabu ilhali Serikali imeshindwa
kuitambua.
Alisema kutokana na kutokuwepo kwa
utaratibu wageni wa nje na ndani hufika bila kizuizi na kujionea maajabu ya
Chemchem hiyo ambayo hutoa maji ya moto pamoja na maajabu mengine yaliyopo eneo
hilo.
“Serikali inatambua uwepo wa
chemchem hii inayotoa maji moto si usiku wala mchana na haina kiangazi wala
masika----raia wa kigeni wanaitambua ila sisi hatuna habari nayo” alisema Hamad
Pinto na kuongeza
“Kama Serikali ingeweka utaratibu wa
kukiweka kituo hiki katika mazingira ya utalii ingeweza kuongeza mapato
yake-----watu wanakuja bila mpangilio na
kupiga picha na kushangaa shangaa” alisema
Kwa upande wake mkazi wa Amboni,
Mussa Juma, alisema kuna vivutio vingi vya utalii eneo hilo lakini
havitambuliki yakiwemo majengo ya kale na misitu yenye wanyama.
Alisema kama Serikali
ingeliviendeleza vivutio hivyo na vijana kupata ajira na kuondokana na ukaaji wa
vijiweni jambo ambalo linawasukuma kujitumbukiza katika viwashawishi.
Alisema vijana wengi hawana kazi na
wamekuwa wakikaa vijiweni hivyo kuwepo kwa vivutio hivyo na kuendelezwa ingweza
kupunguza wimbi la umasikini na ajira kwa vijana.
“Vinaja wengi hawana ajira wala kazi
ya kujiajiri na badala yake wamekuwa wakikaa vijiweni kupiga soga-----kama
vivutio vya kitalii vipo kuna sababu gani ya kuacha kuendelezwa” alisema Juma
Alisema ili kuweza kupunguza
umasikini ni vyema Serikali kuviendeleza vivutio vyake jambo ambalo linaweza kuingiza
mapato na kuweza kupunguza umasikini majumbani.
No comments:
Post a Comment