Tangakumekuchablog
Pangani, WAKAZI
wa Pangani Wilayani hapa wameikumbusha Serikali kuujenga ukuta wa mto Pangani ulioanguka ili kuepusha
kitisho cha maji kuingia mitaani nyakati za upepo na mvua.
Wakizungumza na waandishi wa habari
jana, wakazi hao walisema hadi za sasa hakuna dalili zozote za matumaini ya
kuanza ujengwaji wa ukuta huo jambo ambalo limekuwa likiwapa hofu nyakati za mvua na upepo.
Walisema kwa kipindi kirefu viongozi
wa Serikali wamekuwa wakitoa ahadi ya kujengwa kwa ukuta huo ulioanguka na
kudai kuwa yapata zaidi ya miaka saba na
hivyo matumaini hayo kufifia.
“Tunashukuru nyinyi waandishi kuja
kujionea hatari ya maji kuingia mitaani----ukuta huu umekuwa ukitolewa ahadi na
viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama na leo uoneni hali ilivyo” alisema
Said Khamis na kuongeza
“Kuelekea uchaguzi mkuu tunawaomba
waomba kura kuliweka katika ahadi zai zao huu ukuta kwani hali inazidi kuwa mbaya kila siku
ziendavyo kwani maji yapasua njia kuelekea mitaani” alisema
Wakati huo huo mkazi wa Mkwaja, Ali
Mikidadi, ameitaka Wakala wa ufundi na Umeme kuongea kivuko chengine badala ya cha sasa
kimoja kinachotoa huduma na kuwa kero.
Alisema wafanyabiasha na wafanyakazi
wamekuwa wakichelewa kufika katika maeneo yao ya kazi kutokana na kivuko kuwa
kimoja na hivyo kuchukua muda mrefu kuweza kuvuka kwa wakati.
“Kwa muda mrefu ni kivuko kimoja tu
ndicho kinachotoa huduma na kuwa kero kwa wafanyakazi wa wafanyabiashara-----
wafanyabiashara wa mbogamboga na matunda hufika masokoni muda kuchelewa na kukuta wanunuzi
wameshaondoka” alisema Mikidadi
Alisema ili kuweza kuondosha kero
kwa wakazi wa pande mbili hizo ni vyema Tamesa inayosimamia kivuko hicho kuweka
kivuko cha pili ili kuondosha kero kwa wakazi wa Pangani na maeneo mengine.
No comments:
Post a Comment