Sunday, July 26, 2015

OBAMA HATAZURU KABURI LA BABA YAKE

Obama kutozuru kijiji cha babaake Kenya

Obama  ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo aki wa nchini humo..
Hata hivyo wakazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.
''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa Nairobi pekee'',alisema  Godec akizungumza na runinga ya KTN.
Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.

No comments:

Post a Comment