Saturday, July 25, 2015

KONA ZOTE NI RONALDO NA MTOTO WAKE TU

Cristiano Ronaldo ni kila kona yeye na mtoto wake, mama yake atafahamika? Haya hapa mengine kama yalikupita..

Cristiano-Ronaldo-with-son-Cristiano-Jr-Picture
Cristiano Ronaldo ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania, mara nyingi akiwa anakula good times zake utaona jamaa yuko na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior na huwa anamuwekea ulinzi wa kutosha kila anapokatisha.
241432-06cfd16e-2b7d-11e5-a439-5c856edaa69b
Cristiano Ronaldo Junior alizaliwa June 17 2010 San Diego Marekani wakati ambao Ronaldo alikuwa Afrika ya Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, Ronaldo alitangaza 3 July 2010 kuhusu kupata mtoto kupitia account yake ya Twitter na Facebook siku chache baada ya Ureno kutolewa na Hispania katika michuano ya Kombe la Dunia.
article-1291915-0A51F185000005DC-878_468x339
2920765106
Baada ya Ronaldo kutangaza taarifa hizo za kuwa baba wengi wamekuwa wakijiuliza na kutaka kumjua mama wa mtoto huyo licha ya Ronaldo kutotaka kumuweka wazi baada ya maelezo aliyoandika katika account zake Mitandaoni kwamba hiyo kitu inahusu maisha yake binafsi na haitaji kuweka wazi.
Cristiano+Ronaldo+Junior+Mutua+Madrid+Open+RuGxH5gNub6l
“Nikiwa na furaha tele na hisia za kuwataarifu kwamba hivi karibuni nimekuwa baba wa mtoto wa kiume. Kama nilivyokubaliana na mama wa mtoto kuwa jambo hili kuwa siri. Mwanangu atakuwa chini ya uangalizi wangu. Naomba kila mtu aheshimu haki ya kuwa na usiri angalau kwa masuala binafsi kama haya”>>>Ronaldo
Cristiano+Ronaldo+Cristiano+Ronaldo+Junior+nZyqywCvJgjl
Licha ya kuwa mama wa mtoto hajulikani ila kumekuwa kuna taarifa za kichunguzi amabazo zinasema miezi kadhaa baada ya Cristiano Ronaldo Jr kuzaliwa mama yake alifariki lakini taarifa nyingine zinasema Cristiano Ronaldo Jr alizaliwa na kwa njia za kitechnolojia (Surrogate Mother) ambapo mwanamke wa kimarekani alilipwa na Ronaldo pound milioni 10 ambayo sawa na bilioni 32  za kitanzania ili abebe ujauzito kiteknolojia zaidi.
article-2748033-212DBF6000000578-445_634x632
Ronaldo akimpeleka mwanae shule
Baada ya malipo kufanyika Ronaldo na mama wa mtoto wake wamekubaliana kisheria kuwa asije akajitokeza hadharani na kusema yeye ni mama wa mtoto wa Ronaldo.
24D851B400000578-0-image-a-5_1421740657464

Cristiano-Ronaldo-and-Irina-Shayk
Ronaldo kwenye tuzo za Ballon D’OR 2013 pembeni ni mpenzi wake wa zamani Irina Shayk
PAY-Cristiano-Ronaldo
Cristiano-Ronaldo-and-son-main
29DBB80F00000578-3134686-image-m-57_1434985163084
95da839d88f3d800_101210-cr
Ronaldo aliposhinda goli wakati mwanaye akiwepo uwanjani na kushangilia kwa kunyonya kidole kama mtoto
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment