Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa
Mkoa wa Tanga, Said Magalulla, ameyataka makampuni ya simu nchini kupunguza
gharama za matumizi ya simu ili kuwawezesha watu wa kipato cha chini kuweza
kumudu matumizi ya mitandao hiyo.
Akizungumza mara baada ya kufungua kituo
cha huduma kwa wateja cha kampuni ya simu ya Airtel mjini hapa jana, Magalulla alisema gharama za matumizi ya
simu ziko juu hivyo ni wajibu wa makampuni hayo nchini kumuangalia mtu wa
kipato cha chini.
Alisema asilimia kubwa ya watumiaji
wa simu ni watu wa kipato cha chini
jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa maendeleo ya jamii na kuzidisha ugumu wa maisha.
“Mawasiliano ya simu nchini yanazidi
kukua kwa kasi ila changamoto iko katika gharama za matumizi-----tumeona
gharama zikiongezeka lakini hatuoni zikipungua” alisema Magalula na kuongeza
“Hebu nyinyi airtel tuliopo hapa
onyesheni mfano kwa wengine ili kuiga kutoka kwenu-----kufungua kituo
kikubwa cha huduma kwa wateja hapa kwetu
ni wazi kuwa pato kubwa linatoka kwa mtumiaji tena wa kipato cha chini” alisema
Alisema kituo hicho kitakuwa msaada
mkubwa kwa wananchi wa Tanga na watumiaji wa mtandao wa Airtel na hivyo kuitaka
kuboresha huduma zake zikiwemo za watumiaji wa intareti na simu.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Tanzania,
Adriana Liamba, alisema malengo ya kampuni ya simu ya Airtel ni kumfikia kila
mmoja wa mjini na vijijini na hivyo kuwa na mipango ya kupeleka huduma hiyo
kila pembe.
Alisema mbali ya changamoto kampuni
ya simu inayokumbana nayo lakini imeweza kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali
zikiwemo za kujenga majengo ya shule na zahanati pamoja na vifaa vya elimu kwa
wanafunzi mashuleni.
“Kampuni inakabiliwa na changamoto
mbalimbali kuhakikisha kila mtu inamfikia huduma ya mtandao katika eneo
alilo----ikumbukwe kuwa tumefanya mengi mazuri yakiwemo kujenga majengo ya
shule na vituo vya afya” alisema Liamba
Ameitaka jamii kushirikiana na
kampuni ya Airtel ili kuweza kurahisha maendeleo na ustawi wa uchumi wa nchi na
kila mmoja kufaidika na huduma hiyo muhimu kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalulla, akikata uzi kufungua kituo kipya cha huduma kwa wateja kampuni ya simu ya Airtel kilichopo jengo la Nyumbani Hotel Tanga juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Tanzania kampuni ya simu ya Airtel, Adriana Liamba.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula akiangalia aina za simu ndani ya kituo kipya cha huduma kwa wateja kampuni ya simu ya Airtel iliyopo ndani ya jengo la Nyumbani Hotel. Kilia anaetoa maelekezo ni mkurugenzi mkuu huduma kwa wateja kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Adriana Liamba.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Tanzania, kampuni ya simu ya Airtel, Adriana Liamba, akitoa maelekezo ya shughuli zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalulla ndani ya kituo kipya cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo kilichozinduliwa juzi Tanga.
No comments:
Post a Comment