Haki za binaadamu:Obama aionya Ethiopia
Rais
Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia
amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za
kibinaadamu pamoja na uongozi bora.
Akizungumza katika mkutano na
wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na
waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo
litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika.Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.
Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yalioafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment