Saturday, July 25, 2015

OBAMA AKUTANA NA RUTO ANADAIWA KUWA NA KESI ICC

Obama awazima wengi kwa kukutana na Ruto

Takriban saa ishirini hivi tangu rais wa Marekani Barack Obama awasili nchini Kenya ., Je atakutana na naibu rais wa Kenya  William Ruto au la ?
Naibu rais Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita  baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Kesi dhidi yake inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague Uholanzi.
Wadadisi wa maswala ya kidiplomasia walikuwa wamebashiri kuwa rais Obama asingelikutana naye na atafanya hivyo itakuwa mkutano wa kisiri wala hakutakuwa picha yoyote kwani Ruto angali anatazamwa kama mshukiwa wa makosa jinai.

No comments:

Post a Comment