Van Gaal amzungumzia Ramos, na pia amedokeza juu ya usajili wa mshambuliaji mpya Man Utd
Zikiwa zimebaki wiki takribani wiki 5 kabla ya dirisha la usajili barani ulaya halijafungwa, kocha wa Manchester United – Louis van Gaal amesema kwamba klabu yake ipo sokoni kutafuta mshambuliaji wa kumsajili kabla muda wa usajili haujaisha – huku akisisitiza mchezaji anayemtaka bado hajaandikwa na vyombo vya habari.
Katika
hatua nyingine boss huyo wa Manchester United aliulizwa juu ya tetesi
za usajili wa beki Sergio Ramos wakati wa mkutano wake na waandishi wa
habari, akasema: “Siwezi kuzungumzia tetesi. Nimeshasema kwamba usajili
ni mpango endelevu na labda Mr Ramos yupo katika mpango wetu huo, huwezi
kujua,” alisema kocha huyo wa kidachi.Kwa habari ,matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment