Friday, July 24, 2015

SUNDAY OLISE AMUITA MIKEL OBI WA CHALSEA KUMENYANA NA TAIFA STAR

Kocha wa Nigeria Sunday Oliseh kamrudisha mwingine toka Chelsea ili kujipanga kuivaa Taifa Stars..

Sunday-Oliseh
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa pili wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2017Tanzania ambayo ipo nafasi ya mwisho katika kundi G lenye timu za Nigeria, Chad na Misri inatarajia kucheza na timu ya taifa ya Nigeria September 5 2015 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Oliseh
Kwa upande wa Nigeria ambao wameonesha kujiimarisha zaidi kwa ajili ya mchezo huo, kocha wa timu hiyo Sunday Oliseh akiwa na siku kadhaa toka arithi nafasi hiyo kutoka kwa kocha aliyetimuliwa Stephen Keshi ameanza kutaja nyota atakaowatumia kwa ajili ya mchezo huo.
_60300059_mikel_obi_guinea_gtty
Katika mipango ya Kocha Oliseh, kikosini anatajwa pia kuwepo kiungo wa Chelsea John Obi Mikel ambaye hakuitwa timu ya taifa ya Nigeria tangu November 2014, taarifa kutoka kwa afisa wa ngazi za juu za  soka nchini Nigeria amevujisha stori ya kuitwa kwa Obi.
LUBANGO, ANGOLA - JANUARY 25:  John Obi Mikel of Nigeria during the Africa Cup of Nations Quarter Final match between Zambia and Nigeria from the Alto da Chela Stadium on January 25, 2010 in Lubango, Angola. (Photo by Lefty Shivambu/Gallo Images/Getty Images)
Mikel bado anabakia kuwa moja kati ya nyota wa Nigeria wanaocheza Ulaya licha ya kuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara na Chelsea, hizo ndio sababu za Oliseh kumjumuisha katika mipango yake ya kuanza kuwania nafasi kufuzu kucheza AFCON dhidi ya Tanzania mwezi ujao… Mikel atacheza nafasi ya kiungo mkabaji kama anavyocheza akiwa na klabu yake” >>>> hii ni sehemu ya nukuu kwenye stori za Nigeria ambapo wanasema aliyetoa taarifa ni mmoja ya Viongozi wa juu kwenye Soka Nigeria japo hawakumtaja jina.
Chelsea's John Obi Mikel smiles after scoring a goal against Sporting during their Champions League soccer match at Stamford Bridge in London December 10, 2014. REUTERS/Eddie Keogh      (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER)
Nigeria ipo nafasi ya pili kwa point tatu katika msimamo wa kundi G nyuma ya Misri ambayo ina point tatu na magoli matatu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment