Tuesday, July 21, 2015

SANGOMA ALINENA , YALITIMIA

Mganga aliyetabiri Obama atakuwa Rais wa Marekani, kaja na Utabiri mwingine Kenya..

KENYA
Mzee John Dimo.
John Dimo anafahamika Kenya na hii sio mara ya kwanza kuibuka na utabiri wake, sio kila mtu anaamini kwamba utabiri unatokea kitu kinakuwa kweli, lakini jamaa ana rekodi yake nzuri kabisa yani ndio maana kwenye hii mpya imebidi apewe headlines nyingine.
KENYA II
Obama alitembelea Kijijini kwao Kogelo Kenya mwaka 2006, Mganga akaibuka akasema kwamba Obama atakuwa Rais siku moja, miaka miwili mbele ikatokea kweli… kaibuka tena na kwa maneno yake kabisa kawahakikishia Wanakijiji wa Kogelo kwamba wasiwe na hofu, Rais Obama ni lazima akasalimie ndugu zake pamoja na kutembelea kaburi la baba yake.
Baada ya kufanya vitu vyake vya Kitaalam akaanza kuwapa majibu watu wa Kogelo>>>> “Matokeo inaonesha Obama atakuja Kogelo, ni kwa siri lakini… hakutaka mtu yoyote ajue kwamba atafika Kijijini kwao” >>>> John Dimo.
President Barack Obama ackowledges late-night television host and comedian Conan O'Brien during the White House Correspondents' Association Dinner at the Washington Hilton Hotel, Saturday, April 27, 2013, in Washington.  (AP Photo/Carolyn Kaster)
Rais Barrack Obama.
Akaendelea kuongea kwa watu wake ili kuwaaminisha kwamba Obama ni lazima atue Kijijini >>> “Mniamini, niliwaambia Obama atakuwa Rais na kweli ikatokea… Sasahivi nawaambia atatembelea Kijijini kwao, lazima atakuja” >>> John Dimo.
Rais Obama atatua Kenya Ijumaa July 24 2015 na Balozi wa Marekani Kenya alisema kutokana na ratiba waliyonayo Rais huyo hatoweza kutembelea Kijijini kwao Kogelo.
Tangakumekuchablog itakuhabarisha kila kinachojiri nchini Kenya ujio wa Rais Obama

No comments:

Post a Comment