Hawa ndio wakali wengine watano Ligi ya Uingereza wenye utajiri mkubwa zaidi, na pichaz zao…
Mastaa wa soka wana utajiri wao wa
kutosha tu, unaambiwa kutokana na kazi nzuri wanayoifanya hata thamani
yao inaongezeka vilevile, ukisikia staa wa soka kanunuliwa kwa pound.
Mil 100 Uingereza basi uwe na jibu kabisa kwamba YES jamaa ni jembe la
kazi !!
Lakini thamani yake haiishii uwanjani,
hata nje ya Uwanja jamaa wa Kampuni kama Nike, PUMA, ADIDAS hawamwachii
apite hivihivi wasimpe hata dili moja eti?
Soka na maisha yao nje ya Uwanja
vinasababisha wajikusanyie pesa na wawe na utajiri wa kutosha kabisa…
karibu uipitie hawa watano ambao wametajwa kuwa na utajiri wa juu zaidi
kwenye List ya mastaa wanaochezea Ligi Kuu Uingereza!!
No.5: Utajiri
wake unakadiriwa kuwa kama Dola Milioni 55, umri wake ni miaka 27 tu
lakini tayari kaonesha Ulimwengu jinsi ambavyo ana uwezo mkubwa Uwanjani
kitu ambacho kimempa thamani ya juu pia kati ya mastaa wa Uingereza…
Jamaa anachezea Klabu ya Manchester City.
No.4: Bastian Schweinsteiger, moja ya Vifaa vya nguvu ambavyo vimeenguliwa kutoka Bayern Munich msimu huu na kujiunga na Man United.. Kama akionesha uwezo zaidi basi huenda akapanda chati na kuuongeza utajiri wake ambao kwa sasa ni kama Dola Mil. 60 hivi.
No.3: Japo umri wake ni mkubwa, miaka 34 lakini hata akisema anastaafu leo Klabu ya Chelsea
itakuwa na heshima kubwa kwake kwa mchango mkubwa alioutoa kwa Klabu
hiyo kwa miaka mingi ambayo ametumia akiichezea Klabu hiyo. Yuko vizuri
pia kwenye nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa Dola Mil. 65.
No.2: Yaya Toure ni nafasi ya pili na ndio staa wa Soka pekeake kwenye hii list ya watano ambae ana asili ya Afrika. Utajiri wake ni kama Dola Mil. 75.. Jamaa ni mmoja wa vichwa ambavyo vinategemewa sana Man City.
No.1: Mkali wa Uingereza na mwenyeji wa hapohapo yani.. Kichwa kinachofanya vizuri Manchester United, na ni mmoja ya wakali ambao Uingereza na Man United wanajivunia sana, ukali wake umefanya akae #1 na utajiri wake ni Dola Mil. 110 akimuacha Yaya kwa Dola Mil. 35 hivi !!
Ungana nami kila wakati kupata habari, matukio na michezo papo hapo , ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment