HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI
 Mwakilisha
 wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza
 Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili
 kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama
 kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto 
nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
Mwakilisha
 wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza
 Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili
 kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama
 kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto 
nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog) Kaimu
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline 
Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya 
unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
Kaimu

Imeelezwa
 kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita 
nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa 
kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji 
ya mtoto.
Hayo
 yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, 
Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili 
kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama 
kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
Dkt.
 Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi
 sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali 
sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.
Amesema
 kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na 
mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita 
na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine 
kama uji na maji.
“Hali
 sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa
 ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui 
matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema 
Dkt. Kaganda.
Aidha
 Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa 
kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa 
wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama 
wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze 
kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa 
ya mama yake.
Nae
 Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,
 Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa 
watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama 
wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya
 maziwa ya mama.
Alisema
 watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana 
na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo 
hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya
 Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya 
vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.
“Watoto
 wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na 
kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa 
elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na 
Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,” 
alisema Bi. Zaman.
Alisema
 baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi 
nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya
 mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika 
jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.
Katika
 makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet 
linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza 
kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za 
Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog
 Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa. Mshauri
 Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao 
Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za 
The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya 
mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha 
ya watoto nchini.
Mshauri

ya watoto nchini. Mshauri
 Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao 
Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa
 warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet 
linalohusika na kuandika habari za afya.
Mshauri
 Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao 
Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa
 warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet 
linalohusika na kuandika habari za afya. Viongozi
 wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti 
ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni 
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa 
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya 
Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline
 Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto 
(UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
Viongozi

(UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman. Mkurugenzi
 Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza
 idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
Mkurugenzi
 Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza
 idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto. Viongozi
 wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali
 yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari.
 Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na 
unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, 
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa 
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya 
Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline
 Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto 
(UNICEF) nchini,  Maniza Zaman.

(UNICEF) nchini,  Maniza Zaman. Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo. Mwakilisha
 wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza
 Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha