Sunday, February 14, 2016

MUFTI MKUU WA TANZANIA (BAKWATA) ATOA YA MOYONI

Mufti Mkuu wa Tanzania asifia huduma bora za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu akitoa shukurani za dhati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli mbele ya Mufti Mkuu wa Tanzania pamoja na baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano wa kati siku ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo Jijini Dar es Salaam.
 Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (Kushoto) akitoa shukurani za mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano wakati siku ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA),Sheikh Suleiman Lolila.
 Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Lolila akisoma taarifa ya shukurani toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally mara baada ya kupata matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano Hospitalini hapo wakifuatilia taarifa toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (hayupo pichani) leo katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Jijini Dar esSalaam.

No comments:

Post a Comment