Monday, February 15, 2016

ZIMBWABWE YADAI KUKAMATA NDEGE YA MAREKANI IKIWA NA MAITI NA PESA ZA A , KUSINI

Mamlaka ya anga Zimbabwe yakamata ndege ya kimarekani, kwa kukutwa na maiti na fedha za Afrika Kusini

Mamlaka ya anga ya Serikali ya Zimbabwe February 15 imetangaza kuikamata ndege ya kimarekani inayomilikiwa na Western Global Airlines iliyokuwa imeomba kutua kwa dharura katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare.  ndege hiyo iliyokuwa  inatoka Ujerumani ikiwa imebeba pesa za Afrika Kusini (rand) na maiti.
Ndege hiyo ya mizigo aina ya MD11 iliomba kutua kwa dharura Harare ili ipate msaada wa usalama, lakini ilikuwa inaenda Afrika Kusini  na ilitua Zimbabwe ili kuomba msaada wa mafuta kabla ya kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini. Uchunguzi wa ndege hiyo ulikuwa unaendelea.
Meneja wa mamlaka ya anga ya Zimbabwe David Chaota amethibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo ya kampuni ya Western Global Airlines, kampuni ambayo ipo Florida Marekani, inaripotiwa kuwa ilianza kuomba kutua Msumbiji lakini ilikataliwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment