Friday, February 12, 2016

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA YAFANYA KWELI, TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanga imeteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani zaidi ya shilingi milioni 14  zilizopitwa na wakati katika ukaguzi mpaka wa Horohoro na Kenya pamoja na madukani.
Akizungumza mara baada ya kufanyika zoezi la uteketezaji, Meneja kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA), Dammas Matiko, alisema miongoni mwa vyakula na bidhaa hizo ni  nyama za mbuzi na ng’ombe, vipodozi   pamoja na vinywaji vikali  zikiwemo bia.
Alisema ukaguzi huo ulikuwa na changamoto nyingi zikiwemo wafanyabiashara kukataa kukaguliwa na bidhaa zao kuzificha maeneo ambayo ni vigumu kuonekana kwa urahisi.
“Kwa juma zima tumekuwa tukifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka  hoteli na machinjio, tumefanikiwa kugundua machinjio ya kienyeji mitaani ambayo hayakubaliki ksheria” alisema Matiko na kuongeza
“Ukaguzi huu wa kushtukiza utakuwa endelevu hadi pale tutakapojiridhisha hakuna bidhaa zilizopitwa na wakati na vyama ambazo hazijathibitishwa” alisema
Matiko amewaonya wafanyabiashara kuacha kuagizia bidhaa ambazo zimepitwa na wakati na kusema kuwa sheria haitomvumilia mtu yoyote na badala  yake itawatetea walaji ambao ndio wahanga.
Kwa upande wake Afisa kitengo cha Usalama wa Chakula, dawa na vipodozi halmashauri ya jiji la Tanga, Alice Maungu, amewataka wananchi kuwa na kawaida ya kusoma tarehe za kutengezwa na kuisha muda wa bidhaa anayonunua.
Alisema Watanzania wengi hawana ada ya kujua bidhaa siku iliyotengezezwa jambo ambalo limekuwa likiwaathiri ngozi zao au kuugua magonjwa ambayo chanzo chake ni matumizi ya bidhaa zilizoisha muda wa matumizi.
“Watu wengi hawana kawaida ya kujua bidhaa anayoinunua iko hai au imekufa, hili ni tatizo na ndio maana tunawapa kiburi wafanyabiashara kuagizia bidhaa zilizopitwa na wakati” alisema Maungu
Alisema ni wajibu wa kila mteja anapoenda kununua bidhaa dukani kuangalia tarehe siku iliyotengenezwa na mwisho wa matumizi ikiwa ni kukaribisha  matatizo wakati wa matumizi.
                                                       Mwisho



 Watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga, wakikusanya mapande ya nyama ya ng’ombe na mbuzi zilizokamatwa sokoni na kuzichoma moto jana dampo la Mwang’ombe  baada ya kubainika nyama hizo ziko na magonjwa katika zoezi lilifanywa kwa siku tatu mfululizo kwa usimamizi wa Meneja  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Kaskazini, Dammas Matiko .
 Meneja kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko, akimwaga bia zilizokamatwa katika baa mbalimbali Tanga ambazo zimeisha muda wake wa matumizi zoezi lililofanyika kwa siku tatu mfululizo na kuzitekelezwa dampo la Mwang’ombe jana

Meneja kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko (kushoto) na Afisa Afya kitengo cha usalama wa chakula na dawa halmashauri ya jiji la Tanga, Alice Maungu (kulia) kwa pamoja wakiteketeza makopo ya rangi zilizoisha muda wake wa matumizi dampo la Mwang’ombe Tanga jana







No comments:

Post a Comment