Monday, February 22, 2016

TAPSOA TANGA WACHAGUANA



Tangakumekuchablog
Tanga, UMOJA wa Wamiliki wa Vituo vya Mafuta Tanzania (TAPSOA) tawi la Tanga, limechagua viongozi wake wapya baada wa awali kumaliza muda wake ikiwa ni kushughulikiwa kero na haki za wamiliki wa vituo vya mafuta.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana na kusimamiwa na Katibu Tapsoa Taifa, Tino Massawe, umemchagua, Said Baghozah kuwa mwenyekiti, Amour Ali kutoka kampuni ya GBP kuwa Katibu na Shakir Twaibar kuwa mweka hazina.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya wa TAPSOA Tanga, Said Baghozah, alisema jambo la kwanza ambalo atalifuatilia ni kuomba Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kupunguza gharama za mashine ya mkononi ya DFD.
Alidai kuwa mashine hizo zinazouzwa dola 2,500 ni bei ya juu hivyo baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wenye zaidi ya kituo kimoja hawatamudu gharama za ununuzi hivyo kuiomba kupunguza ili kila mmoja kuweza kununua.
“Mashine za mkono za utoaji risiti ni zuri na lenye tija kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na Serikali, lakini bei iko juu sana na itakuwa vigumu kwa watu wenye vituo zaidi ya kimoja” alisema Baghozah na kuongeza
“Umoja huu nina imani kwanza utawaweka kuwa kituo kimoja wamiliki wa vituo na kuwa na sauti moja katika mambo mbalimbali, tuko na kero nyingi na malalamiko kwa Serikali na Mamlaka ya mapato Tanzania” alisema
Kwa upande wake, Katibu wa umoja huo, Amour Ali, alisema kwa kuchaguliwa kwake kuwa katibu wa TAPSOA tawi la Tanga, wamiliki wa vituo vya mafuta watarajie kuona mabadiliko makubwa sekta ya mafuta.
Alisema kero zote za wamiliki wa vituo vya mafuta atazishughulikia pamoja na mambo mengine yakiwemo kushuka kwa bei ya mafuta na kupanda ambayo imekuwa na misuguano ya mara kwa mara.
“Naomba ushirikiano wenu ili niweze kutimiza yale yote ambayo nimepanga ikiwa ni maslahi kwetu wamiliki na wadau wa mafuta kuanzia Serikali mnunuzi hadi kumfikia mlaji” alisema Amour
Alitoa pongezi kwa viongozi wa Tapsoa Taifa kwa kuweza kushughulikia kero nyingi za wamiliki wa vituo vya mafuta na kuwataka kuzidisha ushirikiano ili kuweza kuleta maendeleo na mageuzi pamoja na mustakbali wa uchumi wa Taifa.
                                                       Mwisho

 Katibu wa TAPSOA Taifa, Tino Massawe, akifungua kikao cha wamiliki na wauzaji wa mafuta mkutano uliofanyika jana Hoteli ya Tangabeach na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa mafuta ndani na nje ya nchi, Dubai, Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)  na kufanyika Tanga


No comments:

Post a Comment