Tuesday, February 16, 2016

WAETHOPIA 13 WATEMBEA KWA SIKU 30 KUISAKA AFRIKA KUSINI WABAMBWA TANGA WAKIWA HOI



Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la Polisi Mkoani Tanga, limewakamata wahamiji haramu 13 wenye asili ya Ethopia waliofichwa msitu  wa Kirare kata ya Pongwe Tanga huku afya  zao zikiwa mbaya baada ya kutembea siku 30 toka waianze safari nchini kwao Ethopia.
Wahamiaji hao ambao wote wamechoka na baadhi yao kushindwa kutembea kutokana na kukaa na njaa na kudai kuwa wamekuwa wakinywa maji ya mito huku madali wao wakiwashindisha na njaa.
Walisema kwa siku zote 30 toka waianze safari wamekuwa wakipita pori kwa pori kuanzia nchini Ethopia , Mombasa nchini Kenya na kuingia Tanzania na kufika mahala kujutia safari yao huku kutojua pa kuanzia safari ya kurejea kwao.
Mmoja wa wahamiaji haramu hao ambaye ndie pekee aliekuwa akizungumza kiarabu alisema wanashukuru askari wa Tanga kwa kuwakamata kwani wameijutia safari yao ambayo jua mvua ni la kwao huku wakishindwa kupata fursa ya kuoga, kupiga mswaki na kulala pahala salama.
Ameitaka Serikali kupitia ofisi ya kamanda wa polisi Tanga kuwarejesha nyumbani kwao ili kuona na familia zao na kujutia kwa madai kuwa hakujua kama safari hiyo itakuwa ya madhila.
Alisema kwa siku zote hizo wamekuwa wakila mizizi na majani pamoja na matunda ya msituni ambayo hawayajui huku madali wao wakiwafuata usiku kila siku wakiwa na maji tu.
                                                Mwisho


















No comments:

Post a Comment