Sunday, February 14, 2016

MANCHESTER CITY YAKUMBANA NA KISIKI CHA MBINGO

Usisahu kuwa Man City wamecheza na Tottenham na kupokea kichapo.

Weekend ya burudani ya soka kwa Ligi Kuu Uingereza ilimalizika usiku wa February 14, kwa jumla ya michezo mitatu kuchezwa kwa siku hiyo, klabu ya Manchester City na Tottenham Hotspurs ndio vilimaliza weekend ya burudani ya soka kwa kucheza mchezo wao katika dimba la Etihad, wakati ambao vilabu vya Arsenal, Leicester City, Liverpool na Aston Villa vilikuwa vimecheza michezo yao weekend hiyo.
2630
Man City ambao walikuwa katika dimba lao la nyumbani, safari hii wamekutana na kichapo goli 2-1 kutoka kwa Tottenham Hotspurs, licha ya kuwa walikuwa kwao, Spurs ndio walikuwa wa kwanza kupachika goli dakika ya 54 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji wao wa kutumainiwa Harry Kane, kabla ya Man City kusawazisha dakika ya  74 kupitia kwa Kelechi Iheanacho, Spurs walifanikiwa kufunga goli la ushindi dakika 7 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa  Christian Eriksen.
2728
Kwa matokeo hayo Sputs wametimiza jumla ya point 51 sawa na Arsenal, ila wao wamefanikiwa kuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli na Arsenal kuwa nafasi ya tatu wakiwa sawa wote wamecheza michezo 26, wakati Man City wapo nafasi ya 4 wakiwa sawa kimichezo na Spurs ila wao wana point 47.
4368
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment