Tuesday, February 9, 2016

RONALDO, MESSI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA FIGO

Real Madrid wameweka wazi mipango yao dhidi ya Ronaldo, Messi kufanyiwa uchunguzi wa figo , atayemrithi Hiddink?

Headlines za soka kutoka Hispania zimenifikia mtu wangu, February 9 naomba nikusogezee TOP 3 stories zilizoandikwa kwa wingi kutoka Hispania. Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Diego Simeone ambaye ni kocha wa Atletico Madrid, majina yao ndio yametumika kupamba headlines za soka February 9.
Msimamo wa Real Madrid juu ya Cristiano Ronaldo
1- Klabu ya  Man United ilikuwa na matumaini ya kumsajili kwa awamu nyingine tena staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ambaye awali ilikuwa inaripotiwa kuwa huenda akahama Real Madrid mwisho wa msimu na kujiunga na klabu ya Man United ya Uingereza au Paris Saint Germain. Ila kocha wa sasa wa Real Madrid Zinedine Zidane amethibitisha kuwa mchezaji huyo hawezi kuondoka Real Madrid, wakati vyombo vya habari vingine vikiripoti kuwa Ronaldo ataendelea kuwa Real Madrid hadi 2018.
cristiano-ronaldo1
Diego Simeone atajwa kuja kumrithi Guus Hiddink
2- Stori nyingine iliyoingia kwenye headlines ni kuhusu kocha wa sasa wa Atletico Madrid Diego Simeone. The Sport Review wanaripoti kuwa klabu ya Chelsea ambayo inafundishwa na kocha wa muda Guus Hiddink hadi mwisho wa msimu, inaripotiwa kuwa Diego Simeone huenda atachukua nafasi ya Hiddink mara baada ya msimu kumalizika.
Diego-Simeone5
Lionel Messi kuendelea na uchunguzi wa figo
3- Klabu ya FC Barcelona ya Hispania stori kutoka sports.ndtv.com inaripoti kuwa klabu hiyo imethibitisha kuwa Lionel Messi anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa figo yake, tatizo ambalo anatajwa kuwa alikuwa nalo toka mwezi December 2015, Messi anaripotiwa kuhudhuria hospitali Jumatatu ya February 8 na Jumanne ya February 9.
lionel-messi-disappointed1
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment