Monday, February 8, 2016

MEMPHIS DEPAY ATUPWA U 21 OLD TRANFORD

Licha ya kusajiliwa kwa dau kubwa, Louis van Gaal kaamua kumshusha U-21 Memphis Depay, kisa ….

Kocha wa Man United Louis van Gaal bado anahangaika kutetea kibarua chake kwa kuhakikisha kuwa timu ya Man United inafanya vizuri, Louis van Gaal anatajwa kuwa katika mikakati ya kuhakikisha Man United inamaliza ikiwa nafasi nzuri, kitendo ambacho huenda kikawafanya viongozi wa Man United kubadili mawazo.
kocha wa Man United Louis van Gaal kaamua kumshusha Memphis Depay katika kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21, Van Gaal amemshusha staa huyo na atacheza katika mchezo kati ya Norwich City usiku huu, lengo likiwa ni kutaka aongeze kiwango kutokana na kutofanya vizuri katika mchezo wa February 7 dhidi ya Chelsea na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
2CCA285A00000578-0-image-a-156_1445127306660
Depay aliyesajiliwa dirisha kubwa la usajili la mwezi wa August 2015 kwa dau la pound milioni 25 akitokea klabu ya PSV Endhoven ya kwao Uholanzi, amekosolewa na wachambuzi na mashabiki wa soka kwa kuonesha kiwango kibovu katika mchezo dhidi ya Chelsea. Depay Jumamosi ya February 13 2016 atatimiza rasmi umri wa miaka 22.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment