Thursday, February 18, 2016

PRISON WAJIFUA KUMENYANA NA MGAMBO TANGA

 Wachezaji wa Tanzania Prison ya Mbeya, wakifanya mazoezi shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga kujiandaa na mchezo wao na Mgambo JKT siku ya Jumamosi uwanja wa Mkwakwani.
Timu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni na kuwavutia watazamaji wengi mjini Tanga.
Wachambuzi wa mambo ya soka Tanga wamedai kuwa Mgambo JKT watakuwa na kibarua kigumu ambapo wengine wamedai kuwa Prison watakiona cha mtema kuni kwani imekuwa ikibadilika na haiaminiki uwanjani na wanaweza kuondoka na point zote tatu.





No comments:

Post a Comment