Tuesday, February 23, 2016

MKURUGENZI KONDOA AKALIA KUTI KAVU


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, amebaini upotevu wa Sh 180 milioni katika halmashauri ya wikaya ya Kondoa mkoani Dodoma,

Kutokana na kubainika kwa upotevu wa fedha hizo Jafo ametoa saa 48 kwa Hussein Issa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kuhakikisha anapeleka maelezo ya kina katika Ofisi ya TAMISEMI juu ya kuibiwa kwa fedha hizo ambazo ni za walipakodi.

Agizo hilo la Jafo lilitokana na ziara yake ya  kikazi iliyofanywa na naibu waziri huyo sambamba na kufanyika kwa kikao cha ndani katika Halmashauri hiyo.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia kiongozi yoyote ambaye atafanya ubadhilifu kwa fedha za Umma au jambo lolote ambalo linaonekana kuwepo kwa  ufisadi.halitavumiliwa.

Amesema nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea na watu kujilimbikizia mali bila kuwa na hofu ya kuhojiwa jambo ambalo liliwafanya watumishi wa Umma kuwa na kiburi na kufanya kile wanachofikiria.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment