Saturday, February 27, 2016

MATUKIO MATATU YA KIHALIFU YALIYOFELI NA KUNASWA NA ASKARI TANGA

 Kamanda wa polisi Tanga, Mihayo Msikhella, akiwaonyesha waandishi wa habari mbinu mpya za wasafirishaji mihadarati aina ya mirungi katika madumu ya maji ili kuficha ushahidi. Madumu hayo ambayo yamekamatwa yakiwa yamesheheni miringi ilikamatwa kijiji cha  Chongoleani Wilayani Mkinga juzi.




 Kamanda wa polisi Tanga, Mihayo Msikhella akiwaonyesha waandishi wa habari wa Tanga, majambazi walivyopiga risasi katika gari ya polisi wakati wa kurushiana risasi baada ya kufanya tukio la Ujambazi Pangani juzi na kuvunja kioo cha mlango wa abiria. Mjambazi hayo yalikimbia na kujificha katika msitu wa Pangani wakitumia pikipiki na hakuna aliejeruhiwa.


 Kamanda wa Polisi Tanga, Mihayo Msikhella akiwaonyesha waandishi wa habari miongoni mwa sukari iliyokamatwa katika bandari bubu ya Kigombe Pangani wakati wa doria iliyofanyika kwa siku mbili mfululizo na kufanikiwa kukamata mifuko 81 ya sukari inayotoka Pakistan, Indonesia na India.


No comments:

Post a Comment