Friday, February 26, 2016

COASTAL UNION YAITUNGUA WAKATA MIWA (MTIBWA SUGAR)

 Timu ya Coastal Union ya Tanga imeitungua timu ya Walima Miwa ya Mtibwa ya Morogoro bao 1 katika mchezo ligi ya FA Cup uwanja wa Mkwakwani leo.
Coastal Unio iliuanza mchezo huo kwa kasi na kusahau kabisa kile kilichodaiwa kuwa mgogoro wa ndani na badala yake walicheza kwa nguvu na kasi na kuwashangaza washabiki walijaza majukwaa mawili uwanja wa Mkwakwani.
Timu ya Mtibwa ilikianza kip[indi cha pili kwa kucheza kwa kasi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kuweza kuingia lango mwa Coastal Unio mara tatu na mashuti yao kupaa juu.

Hadi kipenga cha mwisho Coastal Union ilitoka uwanjani kifua mbele na kocha wa Coastal alisema kuifunga Mtibwa ambayo inafanya vizuri ligi kuu Tanzania Bara Vodacom si kazi rahisi na hivyo kuwaponmgeza wachezaji wake na kuwataka mchezo waliounyesha leo uwe huo huo kwa michezo mengine iliyo mbele yao.


No comments:

Post a Comment