Thursday, February 11, 2016

AJALI YA BASI NA LORI YAUWA WATU 11 TANGA



 Winchi likiking’a kibini ya mbele ya Lori kunasua miili ya watu iliyokwama katika ajali ya basi la kampuni ya mabasi ya Simba Mototo iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam  iliyotokea leo kijiji cha Pangamlima na watu 11 kufariki na wengine 29 kujeruhiwa.




 Sehemu ya mbele ya basi la Simba Mtoto iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam ikiwa imebondeka vibaya baada ya kugongana na lori lililokuwa limebeba mchanga aina ya Krinka utumiakao viwanda vya saruji eneo la Pangamlima Muheza leo ambapo watu 11 walifariki na wengine 29 kujeruhiwa.


  Wananchi na wasafiri  wa Mikoani na Wilayani wakisaidia kunasua miili ya watu walionasa katika lori  na  basi la Simba Mtoto lililokuwa likielekea Dar es Salaam.  lori lililokuwa limebeba mchanga kupeleka Tanga  ambapo watu 11 walifariki na wengine 29 kujeruhiwa vibaya.
  Msururu wa magari yaendayo Mikoani na Wilayani ukiwa umesimama kwa zaidi ya masaa manne kufuatia ajali ya basi la kampuni ya Simba Mtoto na Lori lilikuwa likielekea Tanga kupeleka mchanga aina ya Krinka ajali ambayo ilitokea kijiji cha Pangamlima Wilayani Muheza mapema asubuhi ambapo watu 11 walifariki na wengine 29 kujeruhiwa .


No comments:

Post a Comment