Friday, February 19, 2016

WAZII MKUU ATOA MASAA 20 KUPATIWA TAARIFA YA UNUNUZI WA MATISHARI MATATU BANDARI YA TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amempa masaa 20 Injinia wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Felex Mafinga, kuwasilisha taarifa ya ununuzi wa Matishali matatu badala ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali.
Agizo hilo amelitoka mjini hapa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza bandari ya Tanga, na kugundua matumizi ya pesa ambayo ni tofauti na agizo la Serikali.
Amesema Serikali ilitoa pesa kwa ununuzi wa matishali mawili yenye uwezo wa kufanya kazi masaa 24 na badala ya Mamlaka ya Bandari ikanunua matishali matatu ambayo hayana uwezo na kuhimili upakuzi wa shehena katika meli zinazotia nanga katika kina kirefu cha maji.
Amesema kufuatia kufanywa madudu hayo amemtaka Injia wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Felex Mafinga kuwasilisha taarifa ofisi ya Waziri Mkuu ndani ya masaa 20.
Kwa upande mwengine Waziri Mkuu amewataka Mkuu wa Mkoa, Mwantumu Mahiza, na Kamanda wa Polisi , Mihayo Msikhela, kuzidisha doria mwambao wa bahari ya Hindi ili kuzuia uingizaji wa  Sukari na mali za mgendo.
Alisem Tanga imekuwa kinara wa upitishaji na ushushaji wa Sukari na mali za magendo hivyo kuwataka kuzidisha doria maradufu.
                                        Mwisho

No comments:

Post a Comment