Friday, May 20, 2016

ABAMBWA AKICHUPA UKUTA WA KASRI LA MALKIA WA UINGEREZA

Aliyeingia ndani ya kasri la Malkia akamatwa

Mtu mmoja amekamatwa ndani ya makao ya kifalme nchini Uingereza ya Buckingham baada ya kuvuka uzio wa Kasri
Mtu huyo wa umri wa miaka 41 alipatikana katika uwanja wa kasri hilo dakika saba baada ya ving'ora kuanza kulia siku ya Jumatano jioni.
Mshukiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote alikamatwa kwa kushukiwa kuingia eneo linalolindwa na sasa yuko kizuizini.
Inafahamika kuwa Malkia alikuwa ndani ya kasri wakati wa kisa hicho.
Kumeshuhudiwa utata mara kadha kwenye ulinzi wa kasri la Buckingham miaka ya nyuma, kikiwemo kisa cha Michael Fagan ambaye aliingia hadi chumba cha kulala cha Malkia mwaka 1982, na kukaa kwa muda wa dakika 10 akizungumza na malkia kabla ya Malkia kufanikiwa kupiga king'ora wakati mtu huyo alipoomba sigara.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment