Wahamiaji 700 wafa maji baharini kwa muda wa siku 3
Umoja wa mataifa
unasema kuwa huenda wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika
kipindi cha siku tatau zilizopita katika bahari ya Mediterranean.Wahamiaji waliokololewa kutoka katika boti moja kwenye bahari ya Mediterranea, wamewaambia wafanyikazi wa makundi ya uokoaji kuwa, waliona chombo kimoja cha baharini kilichojaa wakimbizi kikizama.
Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jana Jumamosi.
Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.
No comments:
Post a Comment