Saturday, May 28, 2016

PUNDA KUVALISHWA NEPI KULINDA USAFI WA MAZINGIRA

Punda kuvalishwa nepi Wajir, Kenya

Kaunti ya Kaskazini mashariki mwa Kenya imechukua hatua zisizo za kawaida kulinda barabara moja iliotiwa lami, kwa kuwavalisha nepi punda wanaotumia barabara hiyo.
Mikokoteni yote inayofanya kazi Wajiri sasa italazimika kuweka begi nyuma ya wanyama hao ili kuokota kinyesi chao kwa lengo la kuhakikisha barabara iko safi.
Maderva wa punda hao watalazimika kuwa na Nepi muda wote katika safari zao hasa katika barabara kuu za lami.

No comments:

Post a Comment