Wednesday, May 18, 2016

MTU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ATOA YA MOYONI

Mtu mwenye umri mkubwa zaidi Duniani amezieleza hizi sababu za kuishi maisha marefu

Mwananamama huyo anayeitwa Emma Moran raia wa Verbania Italy ametangazwa hivi karibuni  kuwa ni mtu mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani akiwa na umri wa miaka 116.
Akitoa sababu zake za kuishi muda mrefu zaidi amesema sababu kubwa ni kula mayai mabichi na kutokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, jambo ambalo limeshangaza watu wengi, imesemekana yeye ndiye anaweza kuwa mtu wa mwisho aliyezaliwa karne ya 19 na kuishi mpaka leo karne ya 21.
Akiongea na New York times mwaka 2015 alisema kuwa mayai hayo mabichi anakula mara mbili kwa siku na pia alikuwa na wapenzi wengi hapo awali enzi za usichana wake lakini baada ya kuingia kwenye ndoa isiyo na furaha kwake aliachana na mumewe mwaka 1938 na hakuwahi kuolewa tena………
>>>”Sikutaka kutawaliwa na mtu yeyote na ndio kimenifanya niishi mpaka leo
Bibi huyo amekuwa mtu mwenye umri mrefu zaidi duniani baada ya Susannah Mushatt Jones kufariki siku ya  May 12 2016.
susannah-mushatt-jones
Susannah Mushatt Jones enzi za Uhai wake

No comments:

Post a Comment