Wednesday, May 18, 2016

EGYPT AIR YAPOTEA ANGANI IKIWA NA ABIRIA 56

Ndege ya Egypt imepoteza mawasiliano ikiwa na abiria kutokea Paris Ufaransa

EgyptAir Flight 804 imepoteza mawasiliano ikiwa angani kutokea Paris Ufaransa kwenda Cairo Misri ambako ilitakiwa kutua saa kadhaa zilizopita kwa mujibu wa CNN lakini ikapoteza mawasiliano ikiwa tayari imeingia kwenye anga ya Misri.
Shirika hilo la ndege limethibitisha kwa kusema ilikua na abiria 56 na Wafanyakazi 10 ndani yake ambapo mpaka sasa msako umeshaanza kujua ilipo ndege hii ambayo ilipotea ghafla na kutoonekana kwenye Radar.
Ramani
Ndege hii imepotea ikiwa kwenye umbali wa futi elfu 37 hewani, rubani wa ndege hiyo anao uzoefu wa kurusha ndege kwa saa 6000 huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 4000

No comments:

Post a Comment